- William Ruto aliwaonya viongozi wa kaunti ya Kiambu kukoma kupigana
- Alikuwa akizungumzia mgogoro kati ya Gavana Waititu na naibu wake, James Nyoro
Naibu Rais William Ruto anaonekana kuchukulia agizo kutoka kwa Uhuru kuwa 'anatangatanga' kwa uzito kwani ameonekana akijaribu kunyorosha mambo kadha wa kadha mashinani.
Habari Nyingine: Hawa ndio abiria waliokuwa ndani ya ndege iliyoanguka Aberdares
Ruto alitishia kuwaadhibu vikali viongozi katika kaunti ya Kiambu kama wataendelea na mizozo yao isiyokoma badala ya kushirikiana katika kuwahudumia wenyeji wa Kiambu.

Habari Nyingine: Mwendesha bodaboda aaibishwa kwa kuyakodolea macho makalio ya vipusa
Akiongea mjini Kikuyu siku ya Ijuaa, Juni 8 alipokuwa akiizindua soko la kisasa la Kikuyu ili kupunguza msongamano na kuwapa wachuuzi nafasi za kufanyia kazi, Ruto alisema kuwa vita kati ya viongozi hao ni aibu kubwa.
"Nawaomba viongozi wa eneo hili kufanya kazi pamoja kama ndugu na dada. Hamfai kutumia nguvu zenu nyingi kuleta aibu. Ningetaka muwe timu ya kufanya kazi. Msituletee aibu. Mkiendelea nitarudi na kiboko. Bosi (Uhuru) aliniomba jicho langu liwe kwenu," Alisema Ruto.
Habari Nyingine: Mwanamke aandika CV kwenye mtandao kutafuta mchumba
Huku akiwataka viongozi wakuu; Waititu na Nyoro kufanya kazi pamoja, aliwataka viongozi wa kaunti kufanya kazi kwa karibu na mwakilishi wa wanawake Gathoni Wamuchoba na Seneta Kimani Wamatangi.

Habari Nyingine: Mwanamume afumaniwa akijifanya mwanamke kuwanyemelea wanaume wenzake (picha)
Kama ilivyoripotiwa na TUKO.co.ke, naibu gavana wa Kiambu, James Nyoro alidai kuwa Waititu amekuwa akimtenga katika utendakazi wa kaunti kando na kuwatishia wafanyakazi, akifanya kazi bila ofisi wala gari la serikali.
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibIN0fZBmqa6sn2KutbXSoaCaZZuqxKK7zbKcrKCRYriqwtSmmaJlpp68r7POs6Bmr5FiuKLBza2gZrGRYriqrcybrGadnpmusbuMoZiwmaSWwLa41KGgrKCRYsGwssCuq6Jlqpa8b7TTpqM%3D